• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yanda nafasi 22 kwenye viwango vya soka FIFA

    (GMT+08:00) 2017-04-07 09:18:11

    Magoli yaliyofungwa na Mbwana Samatta, Saimon Msuva na Mbaraka Yusuf waliyofunga wakati Taifa Stars ilipocheza na Botswana na Burundi, imesaidia kuitoa Tanzania shimoni katika orodha ya viwango vya soka vya Shirikisho la Sola la FIFA. Katika orodha iliyotolewa wiki hii, Tanzania imechupa kwa nafasi 22 kutoka 157 mpaka 135, ikiwa siku chache tangu Stars ipate ushindi wa mechi mbili mfululizo wa mechi za kirafiki za kimataifa. Wakati Tanzania ikipanda kwa nafasi hiyo, majirani wa Kenya wamesogea kwa nafasi 10 juu kutoka ile ya 88 hadi ya 78 kidunia, matokeo ambayo yamechangiwa na ushindi kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na sare dhidi ya Uganda.

    Uganda wenyewe wamezidi kuonyesha utemi wao kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kupanda kwa nafasi mbili kutoka ya 74 hadi ya 72 jambo linalowafanya wawe vinara kwa nchi za Afrika Mashariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako