• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuimarisha hatua za kuhimiza hali ya ajira

    (GMT+08:00) 2017-04-07 17:11:07

    Naibu waziri wa raslimali ya watu na utoaji wa huduma za jamii ya China Bibi Zhang Yizhen amesema, hali ya jumla ya watu kupata ajira nchini China katika robo ya kwanza ya mwaka huu ilikuwa tulivu. Ongezeko la idadi ya watu waliopata ajira katika miezi miwili ya mwanzo mwaka huu lilifikia milioni 1.9. Akizungumzia hali yenye utatanishi wa ajira kwa mwaka huu, Bibi Zhang Yizhen amesisitiza kuwa, China itaimarisha sera za kuhimiza utoaji wa nafasi ya ajira.

    Hayo yamesemwa na naibu waziri wa raslimali ya watu na utoaji wa huduma za jamii ya China Bibi Zhang Yizhen katika Mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China. Bibi Zhang ameeleza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, hali ya upatikanaji wa ajira nchini China imekuwa ikidumisha utulivu, na ongezeko la idadi ya watu waliopata ajira mijini na vijijini imezidi milioni 13 katika miaka minne iliyopita, wakati huo huo kiwango cha ukosefu wa ajira katika miji na vijijini kiko chini. Katika robo ya kwanza ya mwaka huu, hali ya upatikanaji wa ajira imedumisha hali yenye utulivu na kuonesha mwelekeo mzuri. Bibi Zhang anasema:

    "Hali ya ajira kwa mwaka huu imeonesha mwelekeo mzuri. Katika mwezi Januari na Februari, ongezeko la idadi ya watu waliopata ajira lilikuwa milioni 1.88, wakati huo huo mahitaji kwa rasilimali watu katika soko pia yanafufuka. Takwimu zimeonesha kuwa, idadi ya mahitaji ya wafanyakazi na watu wanaotafuta ajira zote ziliongezeka katika robo ya kwanza mwaka huu. Idadi ya wanakijiji wanaopata ajira mijini pia imedumisha hali yenye utulivu."

    Hali ya ajira inahusu maisha ya watu wote zaidi ya bilioni 1.3 nchini China. Mkutano wa Baraza la Serikali la China uliofanyika hivi karibuni umethibitisha sera na hatua za kuhimiza utoaji wa nafasi za ajira na ujasirimali kwa hivi sasa na katika kipindi kijacho cha siku za baadaye, ambapo umeeleza bayana kuwa inapaswa kuunga mkono hali mpya ya maendeleo ya ajira, na kupanua sekta za ajira.

    Hali inayofuatiliwa na watu ni kuwa, wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu pamoja na wafanyakazi wanaobadilisha kazi kutokana na upunguzaji wa uwezo wa kupita kiasi wa uzalishaji, pia wamehusishwa katika sera hizo mpya. Mwaka huu idadi ya wanafunzi watakaohitimu vyuo vikuu itafikia milioni 7.95, kiasi ambacho kimeongezeka kwa wanafunzi laki 3 kuliko mwaka jana, na kuweka rekodi mpya katika historia. Bibi Zhang Yizhen ameeleza kuwa, wizara hiyo itachukua hatua mbalimbali ili kuhimiza wahitimu wa vyuo vikuu kupata ajira au kuanzisha biashara. Bibi Zhang anasema:

    "Kutokana na kuwa mashirika ya jamii yana mvuto mkubwa zaidi kwa wahitimu wa vyuo vikuu, kwa mujibu wa sera zilizotangazwa hivi karibuni, mashirika ya jamii yatakayowaajiri wahitimu wa vyuo vikuu yatanufaishwa na sera za kupunguziwa au kusamehewa kodi, kupewa ruzuku za uhakikisho wa kijamii pamoja na dhamana na mikopo inayotumiwa katika uanzishaji wa biashara. Aidha hatua za wahitimu wa vyuo vikuu vya nchi za nje za kuanzisha biashara nchini China zitazidi kurahisishwa."

    Mbali na hayo, mwaka huu China itazidi kuongeza nguvu katika kupunguza uwezo kupita kiasi wa uzalishaji katika sekta za chuma na makaa ya mawe, hali ambayo italeta tatizo la upangaji mpya wa baadhi ya wafanyakazi wa sekta hizo. Sera zilizotangazwa na Baraza la serikali la China zimeamua kuchukua hatua za kutoa ruzuku, na uhakikisho wa ajira ili kukabiliana na hali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako