• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China atoa wito wa kuimarisha mawasiliano na nchi za Afrika kwenye sekta ya ulinzi wa amani

    (GMT+08:00) 2017-04-07 18:15:59

    Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi amesema ni muhimu kuimarisha mawasiliano na uratibu na nchi za Afrika, na kuongeza nguvu ya kuzisaidia, ili kuboresha majukumu ya ulinzi wa amani wa vikosi vya Umoja wa Mataifa.

    Balozi Liu amesema hayo jana kwenye mkutano wa Baraza la usalama kuhusu suala la shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa. Amesema kati ya vikosi 16 vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa, 9 viko barani Afrika, na kati ya nchi kubwa 20 zilizopeleka askari kwenye majukumu ya ulinzi wa amani ya Umoja huo, nchi 12 ni za Afrika.

    Bw. Liu amesema siku zote China inaiunga mkono Afrika kutatua masuala ya Afrika kwa njia ya kiafrika, pia inategemea kuwa Umoja wa Mataifa utapanua na kuzidisha ushirikiano na Umoja wa Afrika kwenye sekta za amani na usalama, na kusikiliza maoni ya nchi za Afrika kwenye sekta ya kulinda amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako