• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mwito kuzuia hali ya Syria isiwe mbaya zaidi

    (GMT+08:00) 2017-04-07 19:39:42

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema, jambo muhimu kwa sasa ni kuzuia hali ya Syria isizidi kuwa mbaya, na kulinda mchakato wa kutatua mgogoro wa Syria kwa njia ya kisiasa.

    Amesema, China inapinga nchi yoyote, jumuiya yoyote au mtu yeyote kutumia silaha za kemikali kwa lengo lolote, na pia inalaani shambulizi la kutumia silaha za kemikali lililotokea nchini Syria. Amesema China inaunga mkono mashirika husika ya Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi kuhusu shambulizi hilo, ili kupata matokeo yanayopimwa na historia na hali halisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako