• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Soka Tanzania-TFF

    (GMT+08:00) 2017-04-10 08:22:01

    Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limetangaza rasmi uchaguzi wake mkuu utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu, uamuzi huo umetolewa na kamati ya utendaji ya shirikisho hilo iliyokutana jijini Dar es salaam jumapili April 9 na kutoa uamuzi huo wa kufanya uchaguzi mkuu siku hiyo Agosti 12.

    Nafasi zitakazogombewa ni za Urais na makamu wake pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji ambao wataunda sekretarieti nzima ya TFF. Katika hatua nyingine, ligi kuu Tanzania Bara itaendelea leo kwa michezo miwili. Mtibwa Sugar wanaikaribisha Azam FC katika uwanja wa Manungu Morogoro, na Mbao FC wanaikaribisha Simba Sports Club katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako