• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakenya wachukua nafasi zote Berlin Marathon

    (GMT+08:00) 2017-04-10 08:22:48

    Wakenya Gilbert Masai na Joan Melly wameng'aa katika makala ya 37 ya mbio za Berlin Half Marathon zilizovutia washiriki 34, 000 nchini Ujerumani wiki iliyopita.

    Masai alikuwa amepigiwa upatu kuibuka bingwa, lakini Melly, ambaye aliingia mbio hizo wa mwisho, hakutarajiwa kabisa kunyakua taji.

    Masai alikamilisha mbio hizo za kilomita 21 kwa dakika 59:57. Alifuatwa Unyuounyo na Wakenya wenzake Vincent Kipchumba na Reuben Limaa, ambao walimaliza mbio kwa dakika 60:32 na 61:43, mtawalia.

    Melly alijumuishwa katika mashindano haya wa mwisho, lakini alivuka utepe katika nafasi ya kwanza kwa dakika 68:45 huku Mkenya mwenzake Edith Chelimo aliridhika katika nafasi ya pili kwa dakika 68:57 naye mzawa wa Kenya, ambaye ni raia wa Uholanzi, Elizeba Cherono akafunga nafasi tatu za kwanza kwa dakika 70:43.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako