• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi kuu Uingereza EPL: Chelsea yajiimarisha kileleni mwa ligi, Manchester United yachupa nafasi ya tano.

    (GMT+08:00) 2017-04-10 08:23:15

    Timu ya Chelsea imeitwanga Bournemouth 3-1 na kurudisha pengo la pointi 7. Bao za Chelsea zilifungwa na Adam Smith aliyejifunga mwenyewe, Eden Hazard na Marcos Alonso. Michezo mingine ilikuwa kati ya Tottenham iliichapa Watford 4-0 na kujisogeza katika nafasi ya pili ya ligi hiyo. Nao Liverpool wakicheza ugenini wameichapa Stroke City 2-1. Huko Etihad, Man City wameweka hai mbio zao baada ya kuitwanga Hull City 3-1. Mechi za jana Manchester United wameicharaza Sunderland bao 3-0 na kukalia nafasi ya tano. Hadi mapumziko Man U walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0 liliofungwa na Zlatan Ibrahimovic. Mchezaji wa Sunderland Seb Larsson alipata kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya Ander Herrera. Mabao mengine ya Man U yalifungwa na Henrikh Mkhitaryan na Marcus Rashford. Ligi hiyo inaendelea leo kwa mechi kati ya Crystal Palace na Arsenal.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako