• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni ya China yatoa msaada wa chakula wa dola 160,000 kwa Kenya

    (GMT+08:00) 2017-04-10 09:33:21

    Ubalozi wa China nchini Kenya pamoja na wachina wanaoishi nchini humo wameendelea kuitikia mwito wa serikali wa kusaidia watu wanaoathirika na njaa.

    Wiki hii msaada uliotolewa na wachina unaendelea kusambazwa katika maeneo mbalimbali yalioathirika.

    Ronalad Mutie anaripoti kutoka Nairobi.

    Msaada huo wa chakula uliotolewa ijumaa na ubalozi wa China pamoja na jamii ya wachina wanaoishi na kufanya kazi nchini Kenya ni wa dola 160,000.

    Msafara wa malori ya chakula hili cha msaada yanaelekea katika kaunti tisa zikiwemo Turkana, Marsabit, Samburu, Lamu, Laikipia, Baringo na Kitui.

    Ingawa mvua imeanza kunyesha lakini bado maeneo kadhaa yanakabiliwa na uhaba wa chakula, maji na lishe kwa mifugo.

    Na hali katika maeneo yenye ukame ni mbaya, wenyeji wanakadiria hasara waliopata.

    "Juzi tumesikia ya kwamba kuna watu wamekufa kwa ajili ya kiu tu upande wa Naisnyono",anasema mmoja wa waathiriwa.

    Msaada uliotolewa ni pamoja na mafuta, unga wa ngano na unga wa mahindi zote tani 144.

    Balozi wa China nchini Kenya Liu Xianfa akiongoza hafla ya kutolewa kwa msaada huo mjini Naiorbi alisema.

    " Kama ndugu na dada watu wa China daima wanasimama pamoja na Wakenya. Serikali ya China ilitangaza kwamba china itatoa msaada wa dharura wa dola bilioni 2.25 kusaida waanga wa janga la njaa.Aidha serikali ya China itatoa mssada wa shilingi milioni 500 kwa wakimbizi wa Somalia na Sudan Kusini wanaoishi nchini Kenya"

    Wakulima na wafugaji kwenye maeneo kadhaa ya kaskazini, pwani na mashariki mwa Kenya hawajavuna chakula cha kutosha kutokan ana kiangazi cha misimu miwili, huku nao mifugo wengi wakiangamia kwa kukosa lishe.

    Mapema mwaka huu rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitangaza ukame kama janga la kitaifa akitoa wito wa msaada kwa jamii ya kimataifa na washirika wa maendeleo.

    Katibu wa kudumu kwenye wizara ya ugatuzi Amani Mabruki anaelezea hali ilivyo.

    "Ukame huu umeathiri zaidi ya wakenya milioni 2.7 ambao kwa sasa hawana chakula. Wanaoathirika sana wako katika maeneo ya majangwa na wengine elfu mia tatu walioko maeneo ya karibu na majangwa"

    Msaada huu wa China unatolewa siku chache tu baada ya china kutangaza kwamba itatoa tani 21 za mchele kulisha waanga wa ukame wapatao milioni 1.4 kwa angalau mwezi mmoja.

    Mchele huo unatarajiwa baadaye mwezi Mei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako