• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa Sweden wamtambua mshukiwa wa shambulizi la lori huko Stockholm

    (GMT+08:00) 2017-04-10 09:37:26

    Polisi wa Sweden wamethibitisha utambulisho wa mshukiwa wa shambulizi la lori kuwa ni raia wa Uzbekistan mwenye umri wa miaka 39, ambaye sasa yuko kizuizini.

    Kamanda wa polisi wa Sweden Bw. Jonas Hysing jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa mshukiwa huyo aliyetuhumiwa kuwagonga watu kwa lori huko Stockholm, na kusababisha vifo vya watu wanne na wengine 15 kujeruhiwa, ameonesha kuwa na uhusiano na kundi la Islamic State.

    Idara ya usalama ya Sweden imesema mtu huyo aliwahi kuomba kibali cha ukazi nchini Sweden lakini alikataliwa mwezi Juni mwaka jana na mwezi Desemba mwaka huo alipewa muda wa wiki nne kuondoka Sweden.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako