• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Algeria na Umoja wa Ulaya kuanzisha utaratibu wa mazungumzo kuhusu kupambana na ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-04-10 17:57:15

    Algeria na Umoja wa Ulaya zimefikia maoni ya pamoja kuhusu kuanzisha utaratibu wa mazungumzo ili kupambana na ugaidi kwa pamoja, na kuongeza maeneo yatakayofanyiwa ushirikiano kupitia utaratibu huo.

    Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya Magreb, Umoja wa Afrika na Umoja wa nchi za Kiarabu wa Algeria Bw. Abdelkader Messahel baada ya kufanya mazungumzo na mjumbe mwandamizi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za diplomasia na usalama Bibi Federica Mogherini aliyekuwa ziarani nchini humo.

    Bibi Mogherini amesema, Algeria ina uzoefu mkubwa katika kupambana na ugaidi na makundi yenye siasa kali, hivyo Umoja wa Ulaya utanufaika kutokana na ushirikiano na Algeria. Bibi Mogherini pia amejadiliana na viongozi wa Algeria kuhusu masuala ya usalama wa kikanda, ikiwemo hali ya usalama ya Libya, Mali na eneo la Sahel, na amesema pande hizo mbili zina msimamo wa pamoja kuhusu kutatua mgogoro wa Libya kwa njia ya amani na kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako