• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: SERIKALI YA PEANA PIKIPIKI 40 KUSAIDIA USAFIRI

    (GMT+08:00) 2017-04-10 20:18:04

    Idadi kubwa ya wakulima nchini Rwanda watafaidika na kuongezeka kwa huduma kupitia pikipiki 40 zilizopeanwa na serikali ili kuongeza uchumi wa kilimo na uzalishaji katika kilimo.

    Mradi huu umeundwa ili kusaidia changamoto ya usafiri inayokabili uchumi wa kilimo nchini Rwanda.

    Jean Claude Kayisinga, katibu mkuu katika wizara ya kilimo, anasema pikipiki zitasaidia kuboresha maafisa wa kilimo kwa safari zao katika maeneo ya vijijini ili kusaidia wakulima kuongeza uzaliashaji wa mazao yao.

    Katika sekta ya kahawa, mpango huu unapanga kuongeza ukuaji wa kahawa kwa asilimia 29 katika mauzo ya nje na kufikia dola milioni 104.3 ifikapo mwaka wa 2018.

    Mradi huu pia unalengo la kuboresha mapato kutoka kwa kilimo cha maua hadi dola milioni 129.6 ifikapo mwaka wa 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako