Bw Li amesema kuwa China na Marekani ni washirika wakubwa wa kibiashara, ambao wanaweza kunufaishana kwa njia ya kukuza ushirikiano. Amesema China inapenda kuhimiza mazungumzo ya makubaliano ya uwekezaji wa pande mbili, na kutatua masuala yaliyopo kwa njia ya mazungumzo, ili kuuhimiza uhusiano wa nchi mbili uendelee kukua kwa uwiano.
Kwa upande wa Marekani, wajumbe wamesema Marekani inafurahia maendeleo ya China, na bunge la Marekani linapenda kuzidisha mawasiliano na China, na kuhimiza urafiki kati ya nchi hizo mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |