• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Familia 560 zaunganishiwa umeme

    (GMT+08:00) 2017-04-11 18:24:26

    Takriban familia 560 katika mkoa wa mashariki mwa Rwanda wamepata huduma ya umeme.

    Hii ni baada ya ushirikiano wa shirika la maendeleo ya kawi nchini humo na Kampuni ya Ignite Power.

    Wafanyibiashara wa mkoa huo wakiwakilishwa na Kamate Cell wanasema watapata fursa ya kuboresha kazi zao pamoja na kuongeza masaa ya kazi.

    Sekta ya jua kali na viwanda pamoja na elimu ni miongoni mwa watakaofaidika pakubwa na mradi huu.

    Familia hizi zimekuwa zikikabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwemo kupanda kwa gharama ya maisha kutokana na kununua mafuta taa kila siku.

    Rwanda inalenga kufikisha matumizi ya umeme kwa asilimia 22 ya raia wake huku serikali ikiendeleza miradi ya umeme wa miale ya jua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako