• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:COTU yataka wafanyikazi kuongezwa mshahara kwa asilimia 22

    (GMT+08:00) 2017-04-11 18:24:40

    Katibu mkuu wa chama cha wafanyikazi nchini Kenya Francis Atwoli ameitaka serikali ya Kenya kuongeza kiwango cha mishahara ya wafanyikazi kwa asilimia 22.

    Atwoli amesema nyongeza hii itasaidia wafanyikazi nchini Kenya kusawazisha hali ngumu ya maisha kutokana na kupanda kwa gharama ya bidhaa na huduma kwa jumla.

    Atwoli amesema wafanyikazi wengi wamekuwa wakilalamikia maisha duni licha ya kupokea mishahara kutoka kwa waajiri.

    Ameitaka mshahara mdogo zaidi wa mfanyikazi wa umma kufikia elfu 15,372 kutoka 12,600.

    Wafanyikazi nchini Kenya wamepongeza juhudi ya katibu huyo kwa kuzingatia matakwa yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako