• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Malipo ya baada ya kustaafu kutolewa kwa siku moja

    (GMT+08:00) 2017-04-11 18:24:54

    Shirika la kitaifa la kuhudumia malipo baada ya kustaafu NSSF la Uganda limebuni mpango mpya wa miaka 10 utakaoboresha huduma zake ikiwemo kutoa malipo kwa waliostaafu kwa siku moja tu kinyume na utaratibu ulioko sasa.

    Katibu wa NSSF Uganda Richard Wabwire amewaambia waandishi wa habari kwamba mikakati kabambe ya mpango huo imeanza na kwamba wamekubaliana mda wa siku 130 kwa mteja kupata mafao yake ni mrefu sana.

    Hii ni baada ya wateja wengi kukosa imani na mafao hayo kwani yamekuwa na vikwazo chungu mzima.

    Maafisa wa NSSF wa Uganda watafanya ziara katika sehemu mbali mbali za wafanyikazi waliojariwa ili kupata maoni ya matakwa yao na vipengee wanavohitaji virekebishwe na shirika hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako