• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makamu wa rais wa China akutana na naibu waziri mkuu wa Namibia

    (GMT+08:00) 2017-04-11 18:46:18

    Makamu wa rais wa China Bw. Li Yuanchao leo hapa Beijing amekutana na naibu waziri mkuu wa Namibia Bw. Netumbo Nandi-Ndaitwah ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo.

    Bw. Li amesema, ushirikiano wa sekta mbalimbali kati ya nchi hizo mbili umepata mafanikio makubwa, na kwamba pande hizo mbili zinaelewana na kuungana mkono katika masuala yanayohusu ufuatiliaji mkubwa na maslahi makuu ya upande mwingine. Amesema China inatarajia pande hizo mbili zitaimarisha uaminifu wa kisiasa, kuongeza mawasiliano kuhusu uzoefu wa utawala wa nchi na ushirkiano wa kunufaishana, na kupanua mawasiliano ya kiutamaduni ili kusukuma mbele maendeleo ya ushirikiano wa kirafiki kati yao.

    Kwa upande wake, Bw. Ndaitwah amesema, anatarajia pande hizo mbili zitaendelea kuongeza ushirikiano katika sekta za utegenezaji, kilimo, mafunzo ya wafanyakazi na mambo ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako