• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Neymar afungiwa mechi tatu na RFEF

    (GMT+08:00) 2017-04-12 09:52:51
    Nyota wa soka wa kimataifa wa Brazil anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Neymar amekutana na adhabu ya kufungiwa mechi 3 kuichezea FC Barcelona na shirikisho la soka Hispania ( Royal Spanish Football Federation (RFEF) kwa makosa mawili.

    Neymar amefungiwa mechi tatu, mechi moja ni kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano wakati wa mchezo dhidi ya Malaga uliomalizika kwa FC Barcelona kupoteza kwa magoli mawili kwa 2-0 lakini mechi ya mbili kwa kosa la kumpongeza kwa kejeli afisa namba nne wakati anatoka nje ya uwanja.

    Mchezaji huyo raia wa Brazil alitoa lugha za kejeli kwa afisa huyo wakati anatoka uwanjani kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano, refa wa mchezo huo Jesus Gil Manzano ndio aliandika ripoti hiyo, Neymar sasa atakosa mchezo dhidi ya Real Sociedad, Real Madrid na Osasuna.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako