• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachezaji saba wa Harambee Stars waondolewa kikosini na kocha

    (GMT+08:00) 2017-04-12 09:53:47
    Wachezaji saba wameondolewa katika kikosi cha Harambee Stars kinachojiandaa kucheza na Malawi. Kocha wa timu hiyo Stanley Okumbi amesema nyota hao wameondolewa baada ya kukosa kufika uwanjani tangu Jumapili kambi ya mazoezi ya timu hiyo ilipoanza.

    Okumbi alisema Paul Kiongera wa AFC Leopards anauguza jeraha, Omar Mbongi (Ulinzi Stars) amejiunga na mazoezi ya kijeshi naye Wafula ameruhusiwa kwenda nyumbani kuomboleza kifo cha mwanawe.

    Kadhalika kocha huyo amewaondoa kikosini wanasoka watano wa Gor Mahia na kuwapa nafasi hizo Brian Birgen wa Ulinzi FC, Victor Majid (Chemilil FC), Zeka Wakoli (GFE FC), Victor Ogedo (Nzoia FC), Shami Mwinyi (Thika United), Ian Otieno (AFC Leopards) na James Saruni wa Ulinzi FC.

    Kikosi cha Malawi kinatarajiwa kuwasili nchini Kenya Jumapili jioni kwa mechi itakayochezwa Jumanne wiki ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako