• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Borussia Dortmund yashambuliwa ikielekea kucheza na Monaco

    (GMT+08:00) 2017-04-12 10:00:52

    Milipuko mitatu imelikumba basi la timu ya Borussia Dortmund lililokuwa likielekea kwenye mchezo wake wa kwanza wa robo fainali ya ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi ya Monaco.

    Katika mkutano na waandishi wa habari mwendesha mashtaka Sandra Luecke, amesema kuwa barua ilikutwa pembezoni mwa eneo la shambulizi hilo, lakini haikuwa na maelezo ya kutosha. Mchezaji mmoja wa Dortmund na raia wa Uhispania Marc Bartra amejeruhiwa na kufanyiwa upasuaji. Msemaji wa klabu hiyo Sascha Fligge amesema Barta anafanyiwa upasuaji kiunoni na wachezaji wengine wote wa timu hiyo wamepatwa na mshtuko mkubwa.

    Milipuko hiyo ilitokea kwenye mida ya saa moja jioni kwa saa huko, mara baada ya basi la timu hiyo kuondoka kwenye hoteli ikielekea uwanja wa Signal Iduna Park.

    Nayo timu pinzani ya Monaco imesema iko pamoja na timu ya Borussia Dortmund katika kipindi hiki kigumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako