• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyakula soko kuu la Mwanza bei juu

    (GMT+08:00) 2017-04-12 19:32:57

    BEI ya vyakula katika soko kuu la Mwanza iko juu ikilinganishwa na hali ilivyokuwa miezi mitano iliyopita.

    Uchunguzi uliofanywa gazeti moja nchini Tanzania imegundua kwamba kutokana na kupanda kwa bei, wanunuzi wengi wamepunguza pia kiwango walichokuwa wakinunua.

    Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko hilo kubwa linalotegemewa na wilaya za Nyamagana na Ilemela, Hamadi Nchola anasema, Novemba mwaka jana kilo moja ya mchele ilikuwa ikiuzwa Sh 1,600, lakini sasa inauzwa Sh 2,000.

    Chakula kingine kilichopanda anasema kuwa ni mahindi ambapo gunia la kilo 100 linauzwa kati ya Sh 120,000 hadi 130,000 kutoka wastani wa Sh 80,000 mwishoni mwa mwaka jana.

    Aidha anasema kupanda kwa bei ya vyakula pia kunawaumiza wafanyabiashara kwa kuwa wateja wanapungua.

    Kilichosababisha bei vyakula kupanda ni ukame ambao umeyakumba maeneo yanayozalisha chakula hizo ikiwa ni pamoja na Mwanza yenyewe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako