• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Benki ya Dunia imeshukisha makadirio ya kiwango cha ukuaji wa uchumi wa Kenya hadi asilimia 5.5.

    (GMT+08:00) 2017-04-12 19:33:36

    Benki ya Dunia (WB) kwa mara nyingine tena imeshukisha makadirio ya kiwango cha ukuaji wa uchumi wa Kenya kwa asilimia 5.5.

    Kulingana na ripoti ya uchumi iliyotolewa jana, wakopeshaji wa kimataifa wanasema ukame, ukuaji wa chini wa mikopo, na bei ya juu ya mafuta itavuta chini ukuaji mwaka huu hadi chini ya makadirio ya awali ya asilimia 5.9.

    Benki ya Dunia inaendelea kusema ukame wa muda mrefu na masuala ya usalama wakati wa uchaguzi bado ni tishio katika uchumi.

    Benki ya Dunia imetoa wito kwa Kenya kuongeza ukuaji wa kilimo na upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi ili kurejesha nchi katika njia ya juu ya ukuaji.

    Uchumi nchini Kenya unatarajiwa kutulia mwaka ujao na Kiwango cha ukuaji wa asilimia 5.8 na asilimia 6.1 katka mwaka 2018.

    Ukuaji wa wastani wa asilimia 5.9 mwaka 2016 kwa kiasi kikubwa ulichangiwa na sekta ya huduma ambayo ilichangia hadi asilimia 3.2 ya kiwango cha ukuaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako