• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vita vya Gor Mahia na FKF vyafungia mastaa nje ya Harambee Stars

    (GMT+08:00) 2017-04-13 09:11:25
    Vita inayoendelea baina ya mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachiel na rais wa FKF, Nick Mwendwa vitakosesha wanasoka wa klabu hiyo ya Gor Mahia nafasi katika kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars kwa ajili ya fainali za CHAN.

    Harambee Stars inajiandaa kupimana nguvu na timu ya taifa ya Malawi maarufu kama Frames katika mechi itakayochezwa April 18 mjini Machakos.

    Naibu Katibu wa klabu hiyo, Ronald Ngala amesisitiza kwamba haitawaachilia wachezaji Boniface Oluoch, Mussa Mohamed, Harun Shakava, Ernest Wendo na Kenneth Muguna kujiunga na timu ya Taifa kwa vile mechi hiyo haitambuliwi na FIFA.

    Kocha wa Harambee Stars Stanley Okumbi amesema mechi hiyo ni muhimu kwavile itasaidia kupima kiwango cha wachezaji wote kabla ya michuano ya CHAN itakayochezwa mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako