• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama cha PKK chatangaza kuhusika na shambulizi la bomu Uturuki

    (GMT+08:00) 2017-04-13 14:17:49

    Chama cha Kurdistan Worker's Party PKK kimetangaza kuhusika na shambulizi la bomu huko kusini mashariki mwa Uturuki.

    Chama cha PKK kimetoa taarifa kwenye mtandao kikisema kwamba mabomu zaidi ya tani 2.5 yametegwa ndani ya handaki lililoko chini ya jengo la polisi katika eneo la Baglar mkoani Diyarbakir.

    Mlipuko ulitokea Jumanne wakati deraya moja lilipotengenezwa ndani ya jengo la kurugenzi ya usalama ya mkoa huo, na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine 12 kujeruhiwa. Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki Bw Suleyman Soylu amelitaja tukio hilo kuwa shambulizi la kigaidi.

    Ofisi ya serikali ya Diyarbakir imetoa taarifa kwamba waasi wa Chama cha PKK walichimba handaki hilo lenye mita 30 kutoka chini ya ardhi ya jengo la makazi hadi karakana ya kutengenezea magari, ili kufanya shambulizi hilo kutoka chini ya ardhi. Watuhumiwa watano wamekamatwa kwa ajili ya uchunguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako