• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Bei ya nyanya na bidhaa nyingine sokoni yapanda Kigali

    (GMT+08:00) 2017-04-13 19:10:20

    Bei ya nyanya mjini Kigali nchini Rwanda imepanda huku kilo moja ikiuzwa kwa franc 900 katika masoko ya Kimironko na Nyabugogo.

    Wiki mbili zilizopita bei ilikuwa ni franc 700.

    Bidhaa nyingine za matumizi ya kila siku zilizopanda bei ni pamoja na viazi na makaa.

    Wachuuzi kwenye masoko hayo wanasema bei imepanda kutokana na kupungua kwa uzalishaji hasa kutoka mkoa wa kaskazini.

    Sasa wafanyabiashara wananunua kitunguu kutoka nchi jirani ya DR congo na hivyo pia kupandisha bei yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako