• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Burundi: Honda Kenya kuuza pikipiki Burundi

    (GMT+08:00) 2017-04-13 19:10:48

    Kampuni ya kutengeza magari ya Honda Kenya inatarajiwa kufungua tawi la kuuza pikipiki nchini Burundi katika mji mkuu, Bujumbura.

    Mwenyekiti wa kampuni hiyo Isaac Kalua amesema tayari wamefikia makubaliano na kampuni ya Old East ya Burundi ambayo inauza pikipiki mjini Bujumbura

    Kalua aliyasema hayo wakati akimkaribisha makamu wa rais wa Burundi Gaston Sindimwo kwenye kiwanda cha Honda katika maeneo ya viwandani mjini Nairobi.

    Sindimwo alisema kuna pikipiki chache nchini Burundi na hivyo kuna fursa kubwa ya kibiashara.

    Alisema kufunguliwa kwa tawi la kuuza bidhaa za Honda mjini Bujumbura kutafungua nafasi za ajira kwa vijana huku matukio ya uhalifu yakitarajiwa kupugua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako