• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito kwa nchi za Maziwa Makuu kushirikiana kiusalama

    (GMT+08:00) 2017-04-13 19:14:03

    Naibu balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Wu Haitao amesema China inazipongeza nchi za Maziwa Makuu kwa kushirikiana katika kukabiliana na tishio linalotokana na makundi yenye silaha, na kuhamasisha nchi za kanda hiyo kuongeza ushirikiano katika sekta ya usalama.

    Akizungumza kwenye mkutano wa wazi kuhusu suala la Maziwa Makuu ulioitishwa jana na Baraza la Usalama la Usalama la Mataifa, Balozi Wu amesema China inapongeza nchi za Maziwa Makuu kutekeleza ipasavyo mpango wa amani, usalama na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC na Maziwa Makuu, na kuhimiza amani na utulivu wa kanda hiyo.

    Hata hivyo amesema nchi za Maziwa Makuu bado zinakabiliwa na changamoto katika kukabiliana na makundi yenye silaha na kutimiza maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako