• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema inafanya kazi zake Mashariki ya Kati bila kuzingatia siasa za kijiografia

    (GMT+08:00) 2017-04-13 19:29:44

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema China inatetea haki za kihistoria na za kimataifa katika suala la Mashariki ya Kati, lakini haizingatii siasa za kijiografia wala kutafuta uwiano katika kanda hiyo.

    Bw. Wang amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Palestina Bw. Riyad Al Malki ambaye yupo ziarani nchini China. Amesema kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuigawa Palestina uliotolewa miaka 70 iliyopita, Israel na Palestina zote zina mamlaka ya kuanzisha nchi, lakini mpaka sasa Palestina bado haijaanzisha nchi yenye mamlaka kamili, na hii si ya haki na inatakiwa kurekebishwa.

    Ameongeza kuwa China inaunga mkono ufumbuzi wa kuwepo kwa nchi mbili za Palestina na Israel na juhudi zote zinazofanywa na nchi zilizo nje ya kanda hiyo ikiwemo Marekani zinazolenga kuchangia utatuzi wa suala la Mashariki ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako