• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Golikipa wa timu ya MC Alger ya Algeria Fawzi Chaouchi adaiwa kwenda jela miezi sita

    (GMT+08:00) 2017-04-14 08:42:05
    Taarifa inayozidi kusambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu golikipa wa timu ya MC Alger ya Algeria Fawzi Chaouchi inawezekana kuwa pigo kwa MC Alger na njema kwa Yanga. Fawzi Chaouchi ameripotiwa kuhukumiwa kwenda jela miezi sita ikiwa siku chache zimesalia kabla ya kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Yanga nchini Algeria. Kwa mujibu wa mtandao wa dzbreaking.com umeripoti kuwa Fawzi aliyecheza mechi ya kwanza ya MC Alger dhidi ya Yanga uwanja wa Taifa Dar es Salaam na Yanga kushinda goli 1-0, amehukumiwa kwenda jela miezi sita na faini ya DA 50.000 kwa kosa la kugombana na polisi. Fawzi anadaiwa kuwa alipishana lugha na kugombana na polisi February 27 baada ya mechi lakini kuna tetesi za chini kwa chini zisizo rasmi zinazodai kuwa taarifa hizo sio za kweli na MC Alger wanajaribu kuwachezea akili Yanga ili waifunge katika mchezo wa kesho.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako