• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazihimiza Marekani na Korea Kusini kusimamisha mchakato wa kuweka mfumo wa THAAD nchini Korea Kusini

    (GMT+08:00) 2017-04-14 18:05:27

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema China inazihimiza tena Marekani na Korea Kusini kusimamisha mara moja mchakato wa kuweka mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora wa THAAD nchini Korea Kusini, na kusisitiza kuwa China itachukua hatua zinazotakiwa kulinda maslahi ya usalama wa nchi na uwiano wa kimkakati wa kikanda.

    Habari zinasema jeshi la Korea Kusini limepeleka vifaa vyote vya mfumo wa THAAD kwenye uwanja wa golf wa Seongju kusini mashariki mwa nchi hiyo, na kusema litajenga mfumo huo mapema ili kukabiliana na tishio la makombora ya nyuklia ya Korea Kaskazini.

    Akizungumzia suala hilo, Geng amesema mfumo huo hautasaidia kutimiza lengo la kutokuwepo kwa silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea wala kulinda amani na utulivu wa peninsula hiyo, na utadhuru vibaya maslahi ya usalama wa nchi husika ikiwemo China na uwiano wa kimkakati wa kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako