• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FKE yalalamikia nyongeza ya mshahara wa chini

    (GMT+08:00) 2017-04-14 20:13:33

    Chama cha waajiri nchini Kenya FKE kimedai nyongeza ya kila mwaka ya mshahara wa chini unaotakiwa kulipwa wafanyakazi umewafanya baadhi ya wawekezaji kukimbilia nhi jirani. FKE inasema hatua hiyo imefanya gharama ya kufanya biashara nchini Kenya kuongezeka kwa asilimia 30 nchini Kenya. Kauli hii inakuja wakati ambapo katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanya kazi nchini Kenya COTU Bwana Francis Atwoli kutaka mshahara wa chini kabisa kulipwa mfanya kazi kuongezwa kutoka shilingi 12,600 hadi 15,372. Hata hivyo FKE inasema baadhi ya wawekezaji wanahamia nchi za Ethiopia, Malawi, Tanzania, Rwanda, Uganda, Malawi na Rwanda ambapo kiwango cha chini cha mshahara kiko chini.Nchini Misri mshahara wa chini kabisa mfanya kazi anatakiwa kuliupwa ni shilingi 6500 huku Ethiopia ikiwa ni shilingi 5000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako