• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matumizi mabaya ya fedha yashuhudiwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-04-14 20:13:50

    Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad ametangaza kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha na mali katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma nchini humo.

    Mbali ya kuwepo kwa ubadhirifu, pia kumekuwa na usimamizi au uendeshaji mbaya wa ofisi na mashirika ya umma hatua iliyoathiri ufanisi au kupunguza tija.

    Hata hivyo, Bw Mussa ameeleza kuimarika kwa makusanyo ya mapato yatokanayo na kodi na yale yasiyotokana na kodi, hatua iliyowezesha serikali kutekeleza bajeti yake kwa kutegemea mapato ya ndani zaidi kuliko kutegemea fedha za wafadhili.

    Kwa upande wa mashirika ya umma, ubadhirifu umeibuliwa katika Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Benki ya Twiga, Benki ya Wanawake, ubia baina ya Shirika la Taifa la Madini (Stamico) na TML, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

    Dosari kwa kundi hilo ambazo zimeathiri uendeshaji wa mashirika ya umma zimebainika katika Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na makampuni ya madini.

    Kwa upande wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, matumizi mabaya ya fedha ulishuhudiwa katika maeneo ya ulipaji wa mishahara hewa, usimamizi na matumizi ya fedha za serikali, usimamizi wa miradi, manunuzi ya umma na ubovu wa mikataba.

    Pia zipo dosari za usimamizi wa mali na madeni ya serikali, uwepo wa mali za kudumu za serikali zilizotelekezwa, ukarabati wa majengo ya serikali na uendelezaji wa viwanja vya serikali katika balozi za Tanzania nje ya nchi na usimamizi wa rasilimali watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako