• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu milioni 14 wa China wachangia damu mwaka jana

    (GMT+08:00) 2017-04-16 16:47:36

    Ripoti iliyotolewa leo na Kamati ya afya na mpango wa familia ya China inasema watu milioni 14 wa China wamechangia damu katika kipindi cha mwaka jana, ambayo ni ongezeko la asilimia 6.1 kuliko mwaka uliopita.

    Ripoti inasema, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, China imejenga vituo 1262 vya kupokea damu na magari 1584 maalumu ya huduma za kuchangia damu Aidha, tume imetoa wito kwa huduma za afya katika ngazi mbalimbali kushughulikia zaidi utendaji wa uchangiaji damu chini ya jina la "kusaidiana"

    Sheria ya kuchangia damu ya China inahamasisha jamaa na marafiki wa wagonjwa kuchangia damu kwa ajili ya mtu mwingine, na imeweka vizuizi kwa mauzo ya damu yanayolenga kupata faida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako