• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya Taifa ya Vijana ya Wanawake ya Kenya yaanza majaribio

    (GMT+08:00) 2017-04-17 08:48:20
    Mazoezi ya majaribio ya kutafuta kikosi cha timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Kenya ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 inaanza leo mjini Eldoret Kaunti ya Uasin Gishu.

    Jumla ya wachezaji 39 watahusika kwenye majaribio hayo ya awamu ya kwanza ambayo ni sehemu ya kutafuta na kuandaa kikosi cha Kenya kitakachochuana na timu ya taifa ya Jordan inayoorodheshwa kuwa nafasi ya 52 duniani huku Kenya ikiwa katika nafasi ya 78 kwa viwango vya ubora vinavyotolewa na shirikisho la soka duniani FIFA.

    Kikosi hicho cha Kenya kitawakilisha Kenya kwenye mechi za kimataifa siku za usoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako