• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • LA LIGA: Barcelona yaifukuzia Real Madrid

    (GMT+08:00) 2017-04-17 08:50:26
    Barcelona wakiwa kwao Nou Camp, wameifunga Real Sociedad 3-2 na kuifukuzia Real Madrid wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na Pointi 75 kwa Mechi 31 na Barcelona ni wa Pili wakiwa na Pointi 72 kwa Mechi 32.

    Wakicheza bila Mastaa wao Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Karim Benzema waliopumzishwa kwa ajili ya Mechi ya Marudiano ya UEFA CHAMPIONS LIGI dhidi ya Bayern Munich itakayochezwa Santiago Bernabeu Jumanne, Real walitoka nyuma kwa Bao la Duje Cop na Isco kuwasawazishia. Magoli mengine ya Madrid yamefungwa na Alvaro Morata na Isco alifunga bao la tatu na la ushindi dakika ya 90

    Huko Nou Camp, mabao ya Barcelona yalifungwa na Lionel Messi bao 2, na Paco Alcacer wakati za Sociedad zilifungwa na Samuel Umtiti, aliejifunga mwenyewe, na Xabier Pieto.

    Wikiendi ijayo huko Santiago Bernabeu, ni ule mtanange mkale uliobatizwa El Clasico kati ya Real Madrid na Barcelona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako