• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 126 wauawa katika shambulizi la mabomu dhidi ya washia Syria

    (GMT+08:00) 2017-04-17 10:43:56

    Shirika la haki za binadamu nchini Syria limesema shambulizi la mabomu dhidi ya msafara wa mabasi yanayobeba washia elfu tano waliokuwa wanaondoka eneo la Rashideen, pembezoni mwa jimbo la Aleppo, limesababisha vifo vya watu 126, wakiwemo wanawake na watoto 80.

    Mshambuliaji wa kujitoa muhanga alilipua mabomu yaliyotegwa ndani ya lori alilokuwa akiendesha kwenye eneo hilo ambako msafara wa mabasi ulikuwa unasubiri kuondoka miji ya Kafraya na Foa na kwenda kwenye sehemu inayodhibitiwa na serikali jimboni Aleppo.

    Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya waasi na serikali, serikali itakubali waasi 2300 na familia zao kuondoka miji ya Madaya na Zabadani, kaskazini mwa Damascus.

    Kazi ya kuhama ilianza Ijumaa iliyopita, lakini washia walipofika katika mji wa Rashideen, walizuiwa na waasi waliotaka kuongeza madai mapya ya makubaliano. Baada ya mlipuko huo, waasi waliruhusu wakimbizi waendelee na safari yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako