• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Bei ya chakula yapanda maradufu

    (GMT+08:00) 2017-04-17 18:53:09

    Bei ya vyakula imepanda kwa kiasi kikubwa kulingana na utafiti wa Newtimes Rwanda.

    Tomato pekee zimepanda bei kutoka Franki 800 hadi 900 kwa kilo.

    Viazi kwa fungu vimeuzwa 350 kutoka 280 hali ambayo sasa imeongeza gharama ya jumla ya maisha.

    Rwanda sasa imeanza kuagiza baadhi ya bidhaa hizo kutoka nchi za nje ili kupunguza kasoro iliyosababishwa na msimu mbaya wa mavuno .

    Mkate ambao ni moja ya aina ya vyakula vinavopendwa nchini humo umepanda hadi franki 1300 baada ya serikali kuongezwa ushuru wa asilimia 18 kutokana na uhaba wa ngano.

    Hata hivyo wafanyibiashara wa masoko ya Kigali wamevuna pakubwa bei hizo kutokana na ongezeko la mahitaji ya chakula kwa msimu wa sherehe za Pasaka.

    Nyama ya ngombe,mbuzi na kuku zimenunuliwa kwa wingi licha ya bei yake kupanda hadi 2300 kwa kilo ya ngombe,2500 mbuzi na 3500 kuku.

    Hali hii imesababisha kupanda kwa mfumko wa auchumi mwezi huu wa Aprili hadi asilimi 7.7

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako