• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Mfumo wa kusimamia fedha wa Ipsis warekebishwa

    (GMT+08:00) 2017-04-17 18:54:49

    Mfumo wa kusimamia pesa za umma kwa njia ya kiteknolojia maarufu kama IFMIS, uliokumbwa na utata katika kaunti sasa umerekebishwa.

    Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Bw Joe Mucheru, alisema hitilafu zilizokuwepo zilikuwa tu changamoto ambazo kwa kawaida hutokea katika ulimwengu wa kidijitali.

    Akiandamana na Katibu wa Wizara hiyo Bw Victor Kyalo na Kaimu Afisa Mkuu Mwelekezi Bw Robert Mugo, waziri alisema utumiaji wa Ifmis ulikwama kwa siku mbili pekee.

    Alitaka kaunti ambazo bado zinatatizika kutumia mfumo huo ziwasiliane na wizara ili ukaguzi ufanywekurekebisha hali hiyo.

    Alikuwa akizungumza pembezoni mwa kongamano la tisa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Hoteli ya Leisure Lodge iliyo Diani, Kaunti ya Kwale.

    Alisema hayo siku moja baada ya Baraza la Magavana kusema mfumo huo ambao hutegemewa kutoa pesa za matumizi ya kaunti ulikuwa haujafanya kazi tangu Aprili 3, na kutatiza shughuli katika kaunti zote 47.

    Magavana walisema malipo ya shughuli muhimu yalitatizwa ikiwemo mishahara ya wafanyakazi na malipo ya miradi muhimu ya maendeleo.

    Kutokana na hitilafu hizo, mishahara ya wafanyakazi ya Machi ilichelewa kulipwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako