• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Wakaazi wataka kuanzishwa kwa Viwanda vya dawa na vifaa

    (GMT+08:00) 2017-04-17 18:55:15

    Wakaazi wa Mwanza wamepewa changamoto ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba kwa kuwa Bohari ya Dawa (MSD) itawapa soko la uhakika.

    Aidha, imeelezwa kwamba kwamba vifaa muhimu vya dawa vinakosekana , MSD inalazimika kuyaagiza Uganda.

    Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakuni, wakati akizungumza kwenye Jukwaa la Biashara jijini Mwanza.

    Alisema kwamba licha ya mkoa wa Mwanza kulima pamba kwa wingi, lakini vifaa vingi vya hospitalini vinavyotokana na pamba yakiwemo mashuka na bandeji, MSD inaagiza kutoka China.

    Alisema kwa sasa Tanzania ina viwanda vitano vya kutengeneza dawa lakini bado vinachechemea.

    Alisema hata yeye anasikitika kwa jinsi pesa nyingi za kununua dawa na vifaa tiba anavyolazimika kuzipeleka nje wakati zingeweza kubaki ndani kama kungekuwa na viwanda vya kutosha vya dawa.

    Tanzania ina Sh trilioni 1.2 kwa ajili ya kununua dawa kwa mwaka lakini sehemu kubwa zinakwenda nje na kufafanua kwamba sehemu kubwa ya pesa hizo zinatolewa na wahisani na sehemu nyingine serikali.

    Alisema moja ya dalili za nchi kutoendelea ni kukosa viwanda vya kuzalisha dawa na vifaa tiba.

    Mbali na MSD, wadau wengine walitoa elimu muhimu kwa wafanyabiashara wa Mwanza ni mabenki ya NMB, TIB (Development), TIB (Corporate) na Benki ya TPB.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako