• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema ni sahihi kutimiza kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea kwa njia za amani

    (GMT+08:00) 2017-04-17 19:15:53

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bw. Lu Kang leo amesema, kutimiza kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea kwa njia zote za amani ni sahihi na pia kunaendana na maslahi ya pande zote husika.

    Akizungumzia kauli ya msaidizi wa rais wa Marekani anayeshughulikia mambo ya usalama ya taifa Bw. Herbert McMaster kuwa, msingi wa Marekani ni kuizuia Korea Kaskazini kutengeneza silaha za nyuklia na kutimiza kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea, Bw. Lu Kang anasema:

    "Kutimiza kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea na kulinda amani na utulivu wa peninsula hiyo kwa mazungumzo na njia ya amani ni njia pekee ya kutatua suala la peninsula ya Korea, na pia ni msimamo ulioshikiliwa na serikali ya China. China inapenda kushirikiana na pande zote ikiwemo Marekani kwa kutimiza malengo hayo"

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako