• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shujaa yapangwa kundi gumu mashindano ya Raga

    (GMT+08:00) 2017-04-18 09:04:29
    Timu ya mchezo wa raga ya Kenya, Shujaa imepangwa katika kundi ngumu la raga za dunia la duru ya Paris Sevens linalojumuisha Uingereza, Ufaransa na Uhispania itakayofanyika Mei 13-14 nchini Ufaransa.

    Ili kufuzu duru zote 10 za raga za dunia za msimu 2017-2018 baada ya kushinda mchujo mjini Hong Kong mnamo April 9, Wahispania walitemwa kutoka raga za dunia baada ya kumaliza msimu wa 2013-2014 katika nafasi ya mwisho.

    Shirikisho la Raga duniani (World Rugby) lilifanya droo ya Paris Sevens baada ya duru ya nane kukamilika nchini Singapore mnamo Jumapili, huku Canada ikitawazwa mshindi wa duru hiyo.

    Kundi A: (Canada, Afrika Kusini, Scotland na Japan), kundi B: (Marekani, New Zealand, Wales na Argentina), huku kundi C lina timu kutoka (Uingereza, Kenya, Ufaransa na Uhispania), na kundi D (Australia, Fiji, Samoa na Urusi).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako