• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UEFA Champions Ligi: Leo nani kutinga nusu fainali?

  (GMT+08:00) 2017-04-18 09:06:41
  Leo na kesho Jumatano usiku mechi za marudiano za robo fainali za UEFA Championi ligi zitachezwa, ili kupata washindi wa kusonga susu fainali.

  Mechi mbili zitakazochezwa leo ni kati ya Leicester City wanarudiana na Atletico Madrid katika uwanja wa King Power, Atletico waliibuka na ushindi wa goli 1-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa wiki iliyopita. Mechi nyingine ni huko Santiago Bernabeu Jijini Madrid kati ya Mabingwa watetezi wa mashindano haya Real Madrid wanapokutana na vigogo wa Ujerumani, Bayern Munich huku Real wakiwa kifua mbele kwa kushinda ugenini Allianz Arena Jijini Munich 2-1 wiki iliyopita.

  Kesho Jumatano pia zipo Mechi 2 kati ya Barcelona na Juventus na nyingine ni AS Monaco na Borussia Dortmund huku Juve wakiwa mbele kwa kushinda 3-0 katika mechi ya kwanza na Monaco pia kushinda kwa Bao 3-2.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako