• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yapanga kuonyesha nyayo mpya za binadamu kwenye majumba ya makumbusho

    (GMT+08:00) 2017-04-18 09:34:43

    Tanzania inapanga kuonyesha nyayo za binadamu wa kale, zilizogunduliwa hivi karibuni katika eneo la Laetoli kwenye hifadhi ya Ngorongoro.

    Mtafiti wa mambo ya kale wa chuo Kikuu cha Dar es salaam Bw Fidelis Masao amesema kazi ya kuonyesha nyayo hizo kwenye jumla la makumbusho itaanza mwezi Agosti mwaka huu.

    Nyayo hizo ziligunduliwa mwaka 2015 na watafiti wa kale wa Tanzania na Italia kwenye shughuli za utafiti na uchimbuaji, kwenye sehemu iliyopendekezwa kujengwa eneo jipya la makumbusho.

    Nyayo hizo zinaweza kutoa takwimu kuhusu mwenendo na ukubwa wa mwili wa binadamu hao wa kale, na kuhimiza utalii unaohusiana na utafiti wa mambo ya kale.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako