• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwekezaji wa China nje ya nchi wapungua katika robo ya kwanza ya mwaka

    (GMT+08:00) 2017-04-18 19:03:40

    Takwimu zilizotolewa leo na Wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, thamani ya uwekezaji wa China katika nchi za nje imepungua kwa asilimia 48.8 katika robo ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.

    Kutokana na takwimu hizo, nchi zilizoko kwenye Ukanda Mmoja na Njia Moja zimevutia zaidi uwekezaji kutoka China, ambapo thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja wa China katika nchi 43 zilizo katika Ukanda huo imefikia dola za kimarekani bilioni 2.95. Uwekezaji huo umechukua asilimia 14.4 katika thamani ya jumla ya uwekezaji wa China kwa nje katika robo ya kwanza ya mwaka huu, na kuongezeka kwa asilimia 5.4 kuliko mwaka jana wakati kama huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako