• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani kuzingatia machaguo yote kwa kuihimiza Korea Kaskazini iache silaha za nyuklia

    (GMT+08:00) 2017-04-18 19:59:01

    Makamu wa rais wa Marekani Bw. Mike Pense aliyeko ziarani nchini Korea Kusini amesema, Marekani inataka kuihimiza Korea Kaskazini kuacha kutumia silaha za nyuklia kwa njia ya amani lakini pia itazingatiamachaguo yote.

    Pense alisema hayo jana baada ya kutembelea eneo lisilo na silaha la Korea Kaskazini na Korea Kusini na kukutana na waziri mkuu wa Korea Kusini Bw. Hwang Kyo-ahn anayekaimu nafasi ya urais na spika wa bunge la taifa wa Korea Kusini Bw. Chung Sye Kyun.

    Akizungumzia kauli ya Pense, Waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov amesema kuwa Russia haioni kama Marekani ina uvumilivu kwa Korea Kaskazini kutokana na mtazamo wa kimkakati. Amesema kama hatua ya Marekani ya kutishia kutumia nguvu dhidi ya Korea Kaskazini kwa upande wake peke yake, italeta hatari kubwa kwa jamii ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako