• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji ya TFF yashindwa kufikia uamuzi wa pointi tatu za Simba Sports Club

  (GMT+08:00) 2017-04-19 09:23:57
  Kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemaliza kikao chake, Katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine, amesema kamati hiyo itakaa tena wiki hii na kuna shahidi wengine wataitwa kuhojiwa baada ya hapo kamati hiyo itatoia maamuzi.

  Kikao hicho kimefanyika jana asubuhi huku waamuzi, wafanyakazi wa bodi ya ligi, viongozi wa simba, Kagera Sugar, waamuzi wa mechi kati ya Kagera Sugar dhidi ya African Lyon na beki Mohammed Fakhi wamehojiwa.

  Awali, kamati ya Saa 72, ilikuwa imeipa Simba pointi 3 na mabao3 licha ya kufungwa kwa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar. Kamati ya Saa 72, ilibaini Kagera Sugar ilimchezesha Fakhi mechi hiyo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba akiwa na kadi 3za njano.

  Lakini Kagera Sugar wakaendelea kusisitiza kwamba Fakhi alikuwa na kadi 2 tu za njano alizopewa katika mechi ya Mbeya City na ile dhidi ya Majimaji na si dhidi ya African Lyon.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako