• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • FINA yamdhamini mchezaji wa Tanzania wa kuogelea

  (GMT+08:00) 2017-04-19 09:24:50
  Shirikisho la mchezo wa kuogelea duniani (FINA) limetoa udhamini wa kambi ya mafunzo ya kuogelea kwa muogeleaji mmoja wa Tanzania, Hilal Hilal ambae amepata nafasi ya kwenda kuweka kambi nchini Thailand kwa muda wa mwaka mmoja.

  Katibu mkuu wa chama cha kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhani Namkoveka na muogeleaji mwenyewe Hilal Hilal wamesema kambi hiyo itamsaidia kufanya vyema kwenye mashindano yajayo ya kimataifa. Mashindano ambayo timu ya taifa ya kuogelea ya Tanzania, itashiriki ni ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika nchini Australia mwakani na yale ya Olympiki yatakayofanyika Tokyo Japan mwaka 2020.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako