• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UEFA Champions ligi: Ronaldo apiga Hat Trick na kuipeleka Madrid nusu fainali.

  (GMT+08:00) 2017-04-19 09:25:42

  Hat Trick za Christiaono Ronaldo zimeiwezesha Real Madrid kutinga nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kuifunga Bayern Munich mabao 4-2. Madrid inakwenda nusu fainali kwa jumla ya mabao 6-3 baada ya ushindi wa mabao 2-1 mjini Munich.

  Bayern walianza kufunga bao la kwanza dakika ya 53 kwa mkwaju wa penalti kupitia Robetro Lewandowski, Madrid wakasawazisha dakika ya 76 akifunga Ronaldo kabla ya beki Sergio Ramos kujifunga dakika mbili baadaye.

  Kipigo cha 2-1 kwa Madrid kilisababisha kuongezwa kwa dakika 30 na ndipo Madrid ilipoanza kuporomosha mvua ya mabao, Ronaldo akifunga dakika ya 106 kwa pasi ya Ramos na Marcelo akawachambua mabeki wanne kabla ya kumpa pasi safi Ronaldo aliyefunga bao la nne dakika ya 110.

  Marco Asensio ndiye aliyefunga bao la nne katika dakika ya 112 na kumaliza kazi dhidi ya Bayern ambao walicheza pungufu kuanzia dakika ya 84 baada ya Arturo Vidal kupigwa kadi nyekundu

  Leicester City yenyewe imeaga michuano hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Atletico Madrid. Kwa sare hiyo, Atletico Madrid imesonga mbele kwa jumla ya magoli 2-1 baada ya ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kwanza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako