• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchakato mpya wa "Mfereji wa Dafa"

    (GMT+08:00) 2017-04-19 17:26:30

    "Mfereji wa Dafa" unajulikana sana katika eneo la milima lililoko mjini Zunyi, mkoani Guizhou, magharibi mwa China. Katika miaka 20 iliyopita, mfereji huo wenye urefu wa kilomita elfu kumi uliochimbwa juu ya mlima mrefu unatumika kwa umwagiliaji kwenye vijiji vilivyoko eneo hilo. Hivi sasa mfereji huo uliokamilishwa kwa kutumia muda wa miaka 36 unapiga hatua katika kipindi kipya.

    Kila siku jambo linalomfurahisha zaidi mwanakijiji wa kijiji cha Mshikamano kilichoko kwenye eneo la Bozhou mkoani Zunyi, ni kuwatunza ng'ombe wa familia yake, kwani ng'ombe wanaweza kubadilisha maisha ya familia ya mkulima huyo anayeishi mlimani.

    "Nafuga ng'ombe kadhaa, na idadi inazidi kuongezeka na eneo la ufugaji linazidi kupanuka."

    Sasa ufugaji wa ng'ombe unaweza kumletea Bw Tang Enju mapato ya RMB yuan elfu 7 hadi 8 kwa mwaka. Katika miaka 20 iliyopita, mapato ya familia yake kwa mwaka mzima hayakufikia RMB elfu tatu. Sababu kubwa ni upatikanaji wa maji, maji hayo yanatoka kwenye "Mfereji wa Dafa" uliochimbwa kwenye mlima ulioko kilomita 10 kutoka kwenye kijiji hicho. Mferejji huo uliopewa na jina la mwongozaji wa ujenzi wa mfereji Huang Dafa, si kama tu umekiletea kijiji cha Mshikamano maji yanayohitajika sana kwa kijiji hicho, bali pia umekiletea matumaini ya kubadilisha kabisa maisha ya huko. Kuanzia umri wa miaka 23 hadi 59, Huang Dafa alitumia maisha yake muhimu katika ujenzi wa mfereji huo, matakwa yake ya mwanzo ni kuwawezesha wanakijiji wenzake kupata wali.

    "Hapo zamani mashamba ya vijiji vyetu viwili yenye eneo la hekta 16 yaliweza kuzalisha kilo elfu 30 tu za mpunga, baada ya kujengwa kwa mfereji huo mashamba yote yanaweza kumwagiliwa."

    Baada ya maji kuingia kwenye kijiji, akiwa mkuu wa kijiji cha Mshikamano, Huang Dafa aliwaongoza wanakijiji wenzake kupanua eneo la mashamba kwa kufuata hali ya ardhi ya milima, na eneo la mashamba ya mpunga limefikia hekta 50, uzalishaji wa mpunga pia umeongezeka kutoka kilogramu elfu 30 hadi laki 4 kwa mwaka.

    Upatikanaji wa maji umeleta matumaini. Wanakijiji wameanza kuanzisha biashara mbalimbali za kilimo na ufugaji kwa kutegemea maji kutoka kwenye "Mfereji wa Dafa". Mwanakijiji Xu Guoshu anayejishughulisha na kilimo kwenye ardhi zenye eneo la hekta 0.8 anasema:

    "Sikutarajia kuwa kuna siku naweza kulima Grapefruit, na kufuga mbuzi na ng'ombe kutokana na ukosefu wa maji. Sasa kuna kituo cha kilimo chenye eneo la hektazipatazo 40, ambacho wanakijiji wanaweza kulima bila malipo, na gharama za usimamizi zinatolewa na serikali."

    Xu Guoshu anakadiria kuwa kilimo cha Grapefruit kinaweza kumletea mapato ya RMB yuan laki 1 kwa mwaka.

    Hivi sasa "Mfereji wa Dafa" unajulikana siku hadi siku, watu wengi wanataka kushuhudia mwujiza huo wa kisasa, na serikali ya huko inapanga kuendeleza utalii katika kijiji hicho. "Mfereji wa Dafa" unapiga hatua katika kipindi kipya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako