• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga kauli yoyote inayoongeza hali ya wasiwasi ya peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2017-04-19 18:54:30

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo amesema, China inafuatilia sana vitendo vya Korea Kaskazini vya kuendeleza silaha za nyuklia na makombora, na kupinga kithabiti kauli yoyote itakayoongeza hali ya wasiwasi ya peninsula ya Korea.

    Bw. Lu Kang amesema, China inashikilia kutimiza peninsula ya Korea isiyo na nyuklia, kulinda amani na utulivu wa peninsula hiyo, na kushikilia msimamo wa kutatua suala hilo kwa njia ya mazungumzo.

    Habari zinasema, naibu mjumbe wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa amesema Korea Kaskazini inafanya maandalizi kwa ajili ya majaribio ya nyuklia. Naibu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo pia amesema Korea Kaskazini itarusha makombora mengi zaidi kila wiki, kila mwezi na kila mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako