• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: China na India ndiyo wameibuka kama wanunuzi wakuu wa mafuta ghafi ya Turkana

    (GMT+08:00) 2017-04-19 19:55:57

    China na India ndiyo wameibuka kama wanunuzi wakuu wa mafuta ghafi ya Turkana ambayo Kenya inapanga kuuza nje chini ya mpango wa majaribio mwanzoni mwa mwezi Juni, kinyume na tangazo lililofanywa mapema kwamba wanunuzi walikuwa wamepatikana Ulaya.

    Watafutaji mafuta kutoka uingereza Tullow, ambao ndio waanzishi wa mafuta Turkana, tayari wamehifadhi mapipa 60,000 ya mafuta ghafi eneo la Lokichar tayari kusafirishwa kuenda Mombasa.

    Bw: Kamau ambaye mwezi Februari alisema walikubaliana na wasafishaji mafuta kutoka Ulaya kununua mafuta ya Kenya jana alikanusha madai hayo na kusema hakuna mkataba wa aina hii ulikuwa umefikiwa.

    Mauzo ya nje ya mafuta ghafi imefungua mstari mpya wa biashara kati ya Kenya na nchi mbili kubwa kutoka Asia, ambazo ni wauzaji wakubwa wa bidhaa Nairobi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako